UFUGAJI WA KUKU WA MAYAI

Kuku wa mayai maarufu kwa jina la LAYES hufugwa kwa minajili wa upatikanaji wa mayai kuku hawa huwa ni jinsia moja tu yaani matete bila majogoo hujirutubisha mayai yake wenyewe kwa kuwapatia chakula chenye virutubisho  vingi kuku hawa huanza kufugwa kuanzia wakiwa vifaranga


HATUA ZA UFUGAJI WA VIFARANGA

Vifaranga vya kuku wa mayai siku ya kwanza unapo viingiza bandani hutengenezwa sehemu maalumu ya kulelea vifaranga inayoitwa bluda humo  huhitaji chanzo cha joto kitakacho dumu kwa muda wa wiki mbili nyuzi joto kwa wiki ya kwanza 35 hadi 30 centigrade  wiki ya pili utafanyika wastani wa nyuzi joto 30 hadi 28.

ULISHAJI WA CHAKULA KWA KUKU WA MAYAI

a) SUPER STARTER wiki ya 1 hadi ya 2

vifaranga wanahitajika kupewa chakula kilaini chenye virutubisho vyote

b) CHIK STARTER wiki ya 3 hadi ya 8

Chakula hiki kimetoutiana kidogo na cha mwanzo hiki si Kilaini sana huanza kumuandaa kifaranga sasa kwa ukuaji wa haraka

c) GROWER MASH wiki 9 hadi 18

Chakula  hiki ndio cha kati cha utayarishaji wa makuzi ya kuku ili kumuandaa kwenda kwenyehatua ya utagaji

e) LAYERS PHASE1 wiki ya 19 hadi ya 40

Chakula hiki sasa ndicho huanza kupewa baada ya kuanza kutaga huanza kutaga kwa asilimia kubwa kama watazingatiwa katika ulishaji

f) LAYERS PHASE2 wiki 41 hadi ya 80

Chakula hiki hupewa wanapofikisha umri huu wanapofikisha wiki ya 60 huanza Kupunguza kasi ya utagaji unashauriwa hadi wanapofikisha wiki 80 ni vyema kuwauza na kuanza na vifaranga

Kuku wa mayai wamegawanyika wapo ambao ni weupe na wenye rangi ya Kidongo chekundu





No comments

Powered by Blogger.