KILIMO BORA CHA BAMIA
Asili ya zao la bamia ni Africa Magharibi zao hili ni miongoni mwa mbogamboga umaarufu wake limekuwa duniani kote katika shughuli za kilimo biashara.
HATUA ZA ULIMAJI WA BAMIA
a) UCHAGUZI WA MBEGU BORA
Ili ulime kiuhakika katika zao hili ni vyema kujua aina za mbegu ambazo ni nzuri katika kilimocha zao hili kuna aina mbalimbali za mbegu zile zenye maumbo makubwa na ndefu nikama (CLEMSON SPINELESS,WHITE VERVET)
b) UCHAGUZI YA ENEO NA MAANDARIZI
Bamiaa huhitaji eneo lenye udogo wa tifutifu ama kichanga ni vyema shamba kutifuliwa vya kutosha kwa kwenda chini ili kuruhusu upandaji wa mbegu kuwa rahisi.
c) UPANDAJI
Bamia hupandwa kwa mstari nafasi kati ya mstari mmoja na mwingine ni CM 60 nafasi kati ya shimo na shimo ni CM 30 kina cha shimo la bamia ni CM 3
d) MATUMIZI YA MBOLEA
Bamia huhitaji mbolea Kama ilivyo mazao mengine jamii ya mbogamboga matumizi ya mbolea ya samadi huongezwa tija katika ukuaji wa bamia wiki moja kabla ya kupanda mbeguni vyema kuweka mbolea kwenye shamba na kuchanganya vyema na udongo.Bamia hukua kwa muda mchache kwa kipindi cha miezi miwili huanza kutoa matokeo ivyo kila baada ya wiki mbili lakini pia kama itaamua kutumia mbolea za viwandani ni vyema kufuata vipimo vya uwekaji katika kila shina.
e) UMWAGILIA WA MAJI
kama utalimaa zao hili kipindi cha kiangazi unashauliwa kumwagia maji ya kutosha mara mbili kwa siku moja asubuhi na jioni
f) ) PALIZI
Shamba la Bamia muda wote linahitajika liwe safi kwa kutoondoa mazalia ya majani husababisha kutokuwa vizuri kwa Bamia
MAVUNO
Bamia huchukua miezi miwili na kuzaa unaweza ukavuna hadi miezi sita
CHANGAMOTO
Usisaha changamoto huwa haikosi ni vyema kuwashirikisha mabwana shamba ukubwani na changamoto za magonjwa.
No comments