KILIMO CHA VITUNGUU MAJI

Zao la vitunguu maji hustawi vizuri kwenye udongo wenye rutuba nzuri.
Udongo wenye kufanya mizizi kupenya kirahisi kama vile wamfinyanzi na tifutifu.
Hali ya hewa inayofaa kwa ajili ya kulima zao hili ni kiasi cha nyuzi joto 22C.
Ili uweze kustawi na kukua vizuri.Zao hili huchukua siku  90 hadi 120


AINA ZA VITUNGUU MAJI
Vitunguu maji vipo vya kienyeji ambazo huthibitishwa na (TOSCI) na vyengine ambavyo ni chotara(Hybrid)
 kama vile;-

(a)red bombay,mangae mola red(VITUNGUU VYEKUNDU)

(b)meru super,tajirika,neptune f1(vITUNGUU VYENYE RANGI YA ZAMBALAU)



HATUA ZA UPANDAJI

Zipo njia mbili za kupanda vitunguu ambazo ni;
(a)upandaji wa moja kwa moja shambani

(b)Upandaji wa kwenye vitalu


CHANGAMOTO ZA UPANDIKIZAJI MICHE YA VITUNGUU MAJI

(i)Mizizi ya vitunguu maji huwa midhaifu

(ii)Upunguza kasi ya ukuaji.


Ila sisi tunakushauri utumie njia ya upandaji moja kwa moja


UAANDAAJI WA SHAMBA LA VITUNGUU

Andaa shamba vizuri kwa kulima na kutifua udongo kwa kina cha sm 35.
weka matuta upana wa m1 huku ukiwa umelainisha udongo vizuri.

NB:hakikisha magugu hayawepo shambani kwa kipindi chote ambacho mimea ipo shambani.


MFUMO WA UMWAGILIAJI

Zao hili huitaji maji kwa kipindi chote cha ukuaji wake.Lakini pia tunashauri kupunguza
umwagiliaji unatakiwa kupunguzwa kadri zao linavyokua.


MAVUNO

Mbegu aina za chotara hukomaa mapema kuanzia miezi 3 baada ya kusia mbegu.
vitunguu maji hutakiwa kuvunwa kwa wakati sahihi ili kuepuka hasara inayoweza kutokana na kuwahi au
kuchelewa katika uvunaji.

No comments

Powered by Blogger.