UTUNZAJI WA SAMAKI AINA YA KAMBALE
Asili ya samaki aina ya kambale ni amerika ya kusini.Samaki huuyu huishi kwenye maji baridi
Barani afrika utafiti unaonesha kiasi kidogo cha uzalishaji wa samaika aina hii kutokana na
ukosefu wa ujuzi wa kitaalamu wa utunzaji wa aina hii ya samaki.
HATUA ZA UTUNZAJI WA KAMBALE
(a)Bwawa/sehemu ya kutunzia
Bwawa la kutunzia kambale inabidi lizingatiwe kwa vipimo maalumu kutokana na idada ya samaki .
mfano;Bwawa la kutunza kambale 1000 huitaji vipimo vifuatavyo {urefu m10,upana m4,na kina cha m1.5}
(b)Mbegu bora ya vifaranga vya kambale
Zipo aina nyingi za kambale kutoka sehemu mbalimbali hukuwa tofauti kutokana na hali ya hewa.
Mfano;African catfish aina hi ya kambale hukuwa vizuri katika nchi nyingi za Afrika na Asia.
;American catfish aina hii ya kambale hukuwa vizuri katika bara la Amerika na Ulaya.
(c)CHAKULA CHA KAMBALE NA ULISHAJI
kambale hula chakula asilimia 10% ya uzito wake.Mfano;Tutauzungumzia wa ulishaji kambale 1000
-mwezi wa 1 kg 30
-mwezi wa 2 kg 60
-mwezi wa 3 kg 120
-mwezi wa 4 kg 195
-mwezi wa 5 kg 255
-mwezi wa 6 kg 345
JUMLA kwa miezi yote hiyo utatumia kg 1005
kwa kipindi cha miezi sita wastani wa kg 2.5 kwa kila samaki.
(d)HEWA YA OKSIJENI
Ufugaji wa kambale wengi katika eneo dogo mfugaji itampasa awe na mashine ya kuongeza
hewa ya oksijeni ndani ya bwawa kwani husaidia ukuaji mzuri wa kambale.
NB;Kwa wale ambao hawana mashine ya kuongeza hewa ya oksijen ni vyema kubadili maji
mara 1 kwa week
HITIMISHO
Kutokana na ongezeko la walaji wengi wa nyama nyeupe hususani samaki,Hii imepelekea kuhitajika kwa wingi sokoni
na hivyo kufanya soko la samaki kuwa kubwa duniani kote hivyo kupelekea mfugaji kuwa na soko la uhakika.
No comments