KILIMO CHA MATIKITI MAJI


Matikiti maji ni moja ya mazao ya matunda ambayo ni rahisi sana kuzalisha na lisilohitaji gharama kubwa .
Gharama ya kulima ni kuweza kufahamu mazingira yanayofaa kwa ajili ya tikiti maji,
uchaguzi sahihi wa mbegu,upandaji,matunzo na mambo mengine machache ya muhimu na yasiyo na gharama kwa mkulima.

Zao hili hulimwa sehemu nyingi duniani zenye hali ya hewa ya joto la wastani.
Katika shamba la ukubwa wa hekta 1 lililoandaliwa kwa utaalamu unaoelekezwa na mabwana shamba.
Mkulima ana uwezo wa kuvuna kiasi cha TANI 50!Hivyo faida ipo tena nzuri.


 KUNA AINA MBILI(2) ZA MATIKITI MAJI

(a)Matikiti maji yenye rangi ya kijani :-Huwa na umbo kubwa na mwonekano wa duara

(b)Matikiti maji yenye rangi ya mabaka mabaka:-Yana umbo la wastani na kimo kirefu.



 UANDAAJI WA SHAMBA

Shamba lisafishwe vizuri na litifuliwe kwa kiasi cha inch 9 kwenda ardhini.
Kwa ukubwa wa shamba la hekta 1 kiasi cha mbegu KG 4 hutumika.



UPANDAJI

Tunashauri usipande kwenye kitalu kutokana na miche ya matikiti huwa ni dhaifu
wakati wa upandikizaji shambani.Matikiti hupandwa mbegu mbili kwenye shimo moja.
Matikiti maji kaiikka hatua ya kutoa matunda tunashauri kupunguza matunda ili kupata
matunda yenye ukubwa ambayo utakuwa na uhakika wa soko kibiashara.



MATUMIZI YA MBOLEA

Tunashauri kabla hujafanya matumizi ya mbolea hakikisha umepata vipimo sahihi
vya udongo husika.Hii itakuwezesha kujua wingi wa madini au uchache wa madini na
kufanya matumizi sahihi kwa wakati.
Matikiti maji huitaji mbolea zenye nitrogen kidogo yakiwa katika hatua za awali.
Mimea ikishaanzaaa kutoa maua tunashauri utumie mbolea zenye mchanganyiko wa nitrogen pamoja
na madini ya boron.Tumia mbolea zenye potassium mara 1 kwa wiki hadi matunda yatakapo komaa.



MATUMIZI YA MAJI/UMWAGILIAJI

matikiti maji huitaji maji zaidi kipindi cha uotaji wa mbegu,utoaji wa maua.
Epuka kumwagilia wakati wa jionii na usiku kwa sababu hupelekea tatizo la majani kutokana na unyevu
kukaa muda mrefu.
Upungufu wa maji husabisha kutengenezwa matunda ambayo yenye umbo baya.

WADUDU WAHARIBIFU NA JINSI YA KUWADHIBITI

Matikiti maji hushambuliwa na wadudu ambao hukaa katika majani,maua na matunda.
Dawa ambazo huangamiza wadudu hawa ni pamoja na actara,ninja,dudu all,abernil,farmerguard



JINSI YA KUDHIBITI MAGONJWA

Ni vigumu sana kuzalisha zao hili wakati wa msimu wa mvua, hivyo inashauriwa kupanda wakati wa kiangaz.
Ugonjwa wa Ubwiri unga hushambulia zaidi matikiti maji.Hivyo tunashauri kuudhibiti ugonjwaa mapema tokea
hatua za awali.


MAVUNO

Tikiti maji huwa tayaari kuanza kuvunwa baada ya siku 75 kwa mbegu hybrid  f1 na siku 90 kwa mbegu za asili.


No comments

Powered by Blogger.