UTENGENEZAJI WA CHAKULA MBADALA KWA MIFUGO

Ili ufanye ufugaji wenye tija na kuweza kupunguza gharama  kubwa za ulishaji wa mifugo kama kuku,ngo'ombe, mbuzi na kadhalika yatupasa kutambua mbinu nzuri itakayokufaa kiulishaji na isiyoghalimu kwa kiasi kikubwa kiuchumi wa pesa kitaalamu uzalishaji huu wa chakula mbadala wanaiita (HYDROPONIC FODER) hutumia mbegu za nafaka

MAHITAJI

a) Mbegu za mtama

b) Mbegu za shairi

c)  Mbegu za mahindi

VIFAA VYA KUOTESHEA

 1)TREI maalumu kwa ajili ya uotesheaji treni ziwe na vitundu vidogodogo kwa chini zitakazoruhusu maji kutokutuwama hii itasaidia wakati wa kumwagilia kutokuoza kwa mbegu

2)CHUPA hutumika katika umwagiliaji unaposiha mbegu kwenye trei katika umwagiliaji kwa kutumia chupa ambayo imetolewa juu ya mfuniko vitundu vidogodogo inasaidia kulowanisha mbegu kiufasaha na zote kupata maji

UHIFADHI KATIKA  UKUAJI

Hifadhi sehemu yenye mwanga kiasi isiyopigwa na jua la moja kwa moja lakini panahitajika pawe hewa ya kutosha kuruhusu ukuaji mzuri

UPANDAJI

Robo ya mtama ukipanda hutoa uzito wa KG 1

UMWAGILIAJI

umwagiliaji huwa kama kilimo kingine unabidi imwagike asubuhi na jioni

UVUNAJI

huanza kuvunwa kuanzia siku ya saba jinsi zinavyozidi ongezeka ndio huzidi kuwa kwa ukubwa


No comments

Powered by Blogger.