CHAKULA CHA KUKU KIENYEJI NA KUKU CHOTARA

KUKU kienyeji na KUKU chotara wanatofauti mdogo sana KUKU wa kienyeji ingawa wanasifa zilizolingana kwa kiasi kikubwa hivi ndivyo ilivyo ata katika ulishaji wa chakula unashabiiyana.


Ukuaji wa kuku hutegemea chakula bora kwa asilimia 70 sasa ni njia zipi unaotakiwa kufuata kuanzia unapoanza kufuga kuku akiwa bado kifaranga hadi inapofikia hatua ya kumuua ama kujipatia kitoweo.

1)Siku ya kwanza unapoingia vifaranga vyako vya kuku viwe vya kienyeji ama vya chotara
inabidi uwape chakula aina ya STASTER hiki ni chakula maalumu kwa ajili ya vifaranga vifaranga hupewa ndani ya mwezi mmoja.Mfano vifaranga 100utavipa KG 75  ndani ya mwezi mmoja unashauliwa kama unataka kufuga kibiashara ili kuona matokeoya ukuaji kwa haraka ni vyema kuwapatia vifaranga vyako chakula usiku na mchana

MCHANGANYIKO WA CHAKULA CHA STATER

a) Unga wa dona 20
b) Mahindi yaliyopalazwa KG 10
c) Pumba za mahindi KG 10
d) dagaa waliosagwa KG 15
e) Chumvi nusu KG
f) Mashudu ya alizeti KG 10
g) Chikpremix  robo KG
h) Unga wa mifupa KG 10


MCHANGANYIKO WA CHAKULA CHA MIEZI 2 HADI 4

a) Pumba za mahindi KG 15
b) Mashudu ya alizeti KG 10
c) Chumvi robo KG
d) Unga wa mifupa KG 5
f) Damu KG 5
g) Dagaa KG 10
h) Soya kavu 10
i) Mahindi paraza KG 20
j) Unga wa dona au mtama KG 10

CHAKULA KUKU WANAOTAGA  MIEZI 5 NA KUENDELEA

a) Mapumba KG 10
b) Mahindi yaliyo parazwa KG 20
c) Mashudu ya alizeti KG 10
d) Mifupa KG 5
e) Soya kavu KG 5
f) Dagaa KG 15
g) Chumvi nusu KG
h) Layersprimix robo KG


1 comment:

  1. Akhasante kwa maelekezo kwa mimi natamani sana KILIMO cha vitunguu mnabisaidiaahe

    ReplyDelete

Powered by Blogger.