KILIMO CHA MAPAPAI

Papai ni moja kati tunda pendwa ambalo kwa kiasi kikubwa watu wengi hutumia kiafya linafaida  mbalimbali hivyo nchi nyingi hulika zao hili hasa zile nchi zenye  hali ya kitropiki.

UCHAGUZI WA  MBEGU ZILIZOBORESHWA

Mbegu  za papai zipo za  aina tofauti tofauti na huwa na sifa za kipekee kwa kila moja

a) MALIKIA f1

hii ni mbegu maarufu sana kutokana kuwa na matokeo  mazuri  kama utahudumiwa vizuri  katika  mbegu hii hutoa matunda yenye maumbo makubwa ndani yake huwa na sukari kwa kiasi kikubwa

mbegu nyingine ni kama

b) CALINA

c) RED ROYAL

c) AFRICAN PAPAYA

UANDAAJI WA MBEGU  KWA AJILI YA KUOTESHA

mbegu za papai hukaushwa vizuri kwa mwanga wa jua baada hapo zikiwa kavu kabisa hulowekwa ndani ya maji kwa muda wa siku mbili unashauriwa kila baada ya masaa tisa kubadili maji na kuweka maji mengine safi.

MATUMIZI  YA MBOLEA  KWENYE KITALU

Tumia mbolea ya samadi andaa mbolea changanya na udogo vizuri wiki moja kabla ya kuweka mbegu kwenye kitaru

UPANDAJI WA KWENYE KITARU (VIRIBA)

Baada ya siku mbili mbegu hutolewa katika maji kwa ajili ya kuotesha katika kitalu jinsi ya kupanda mbegu kwa kila kiriba kimoja urefu wa nusu centimenta mbegu huchukua muda wa siku 8 hadi 10 kuota kwenye kitalu

UMWAGILIAJI WA MAJI KATIKA  KITALU

Mwagilia maji mara mbili kwa siku asubui na jioni usimwagilie maji yenye presha kubwa utasababisha kutoka kwa mbegu nnje ya viriba

KUHAMISHA MICHE YA PAPAI

Miche ya papai huanza  kuhamishwa wiki ya pili hadi ya tatu tangu kuota kwake na kuwekwa shambani.

UPANDAJI  KATIKA  SHAMBA

Chimba mashimo yenye umbali kati ya shimo na shimo mita moja kina cha kwenda chini katika shimo la mpapai CM 50 na mapana ya shimo CM 30

UMWAGILIAJI WA MAJI KWENYE SHAMBA LA MIPAPAI

katika  hatua hii mpapai unahitaji maji ya kutosha na kwa wakati mwagilia kutokana na ukuaji wake wiki ya kwanza hadi ya nne  baada ya kupandikiza  mwagilia lita tatu kila mche asubuhi na jioni kama ni kipindi cha jua kari

MATUMIZI YA MBOLEA KWENYE SHAMBA

Ili uweze kupata ukuaji wa haraka na wenye kutoa matokeo mazuri mbolea huchukua nafasi katika ukuzaji baada ya kutowa miche katika kitalu na kupandikiza shambani kwenye kila shimo utakalo pandikiza  papai linahitaji mbolea unaweza tumia mbolea za asili kama samadi lakini pia unaweza tumia. Mbolea za viwandani ambazo utashauriwa kwa vipimo maalumu katika matumizi yake kama utatumia samadi utaongeza kila baada ya wiki mbili.

CHANGAMOTO  ZA MAGONJWA

Kilimo cha mapapai inachangamoto zake mbalimbali imeshauriwa ukiona dalili zozote  zile ambazo zinaashiria ukuaji  wa mipapai waone mabwana shamba ama fika maduka ya pembejeo kwa ushauri dawa gani zuri kutumia kutokana na dalili husika.

MAVUNO

Mipapai huanza kuvunwa baada ya miezi mitano hadi sita hudumu kwa muda wa miaka miwili

No comments

Powered by Blogger.