KILIMO CHA PILIPLI MBUZI
Pilipili mbuzi ni zao ambalo linaweza kulimwa kibiashara na kumpatia faida nzuri mkulima. Zao hili huitaji mwanga wa kutosha wa jua angalau kiasi cha masaa 6 kwa siku.
Pilipili hustawi vizuri zaidi kwenye udongo wenye mbolea ya asili, undongo wenye unyevu nyevu ila usiwe wenye kutuamisha maji.
Pilipili mbuzi huitaji udongo wenye pH 6.0 hadi 6.8, Ikiwa PH ni chini ya 6.0 ongezea madini chokaa kwenye udongo; Na ikiwa pH ya udongo imefika 8 onana na wataalam wa kilimo wakusahuri namna ya kuipunguza.
Kuandaa miche.
Mbegu za pilipili huoteshwa miche kwenye kitalu kabla ya kwenda kupandikizwa shambani. Pandikiza mbegu kwenye kitalu week 7 hadi 10 kabla ya kipindi ambacho umepanga kupandikiza miche shambani. Panda mbegu tatu tatu kwenye kila kishimo na chagua mbili zilizo chipua vizuri kwa ajili ya kuhamishia shambani.
Kuhamishia miche shambani.
Hamisha miche shambani ikiwa imetengeneza majani 8, ingawa kuhamisha ikiwa na majani machache au mengi zaidi haitapelekea shida yoyote.
Uhamishaji wa miche shambani kama mkulima Unashauriwa kuzingatia mambo yafuatayo.
- Siku ya kwanza kwa lisaa limoja weka miche kivulini au mahali ambapo kuna kizuizi jua la moja kwa moja lisiifikie miche. Kadri siku zinavyo kwenda ruhusu miche kupata mwanga wa jua zaidi.
- Changanya sulphur (Tembe 2) kwenye maji na kumwagilia na rudia mchanganyo huu kila baada ya week mbili. Sulphur husaidia kuuwa fungus, inauwa bacteria wasio faa, kuzuia magonjwa pia huasaidi mizizi kusambaa na kukua kwa haraka na kupata virutubisho.
- Mwagilia miche maji ya kutosha baada ya kuihamishia shambani hiyo husaidia kupunguza stress za mmea unapobadilishiwa mazingira. Tumia mbolea ya Miracle Gro kila baada ya week mbili.
Mahitaji ya mmea.
Pilipili ni zao lenye kuhitaji zaidi unyevu unyevu shambani ila maji yasiwe yenye kutuama. Kipindi ambacho maua yametoka na vitunda vya pilipili vimeanza kujitokeza, udongo ukiwa mkavu sana hauna unyevu wa kutosha hupelekea maua kudondoka. Epuka umwagiliaji ulio zidi mahitaji au ulio chini ya mahitaji. Unaweza kutandaza nyasi kwaajili ya kusaidia kuhifadhi unyevu shambani. Mmea huanza kutoa maua mapema baada ya kutengeneza matawi, Maua ya mmea hua na set iliyo kamilika (jike na dume) hivyo kuwa na sifa ya kuweza kujichavusha yenyewe.
Upepo, wadudu au kwakutumia mkono husaidia kuongeza uchavushaji.
Mbolea
Siku 10 Baada ya kupanda sasa endelea kukuzia mbolea,wakati huu tumia ya mboji 5-10g kwa mche.NB:Usitupie juu..hakikisha mbolea unaifukia kuzunguka mmea na usiweke karibu sana na mmea,weka 4-6 cm kutoka kwenye mmea.
Kupalilia.
Pilipili zi zao ambalo halina mizizi merefu sana, hivyo basi mkulima anapaswa kuzingatia hilo na kuongeza umakini wakati wa kupalilia kuepuka kukata mizizi.
Magonjwa.
Fusarium wilt (Mnyauko)
Njinsi ya kuepuka. .Tandika shamba lako na majani makavu ili kupunguza joto.Southern blight ( Sclerotium wilt)
Huu ungonjwa utaona kwenye shina china panaota fangasi weupeweupe (Whitish fungal growth on the stems of infected plant) .Majani ya chini huweza kunyauka,Huu ungonjwa hutokea muda mfupi kipindi cha joto kali.
Kuepuka/Kuzuia.
.
Huu ni ugonjwa wa kawaida kwenye pilipili mbuzi na huu ugonjwa huweza kukaa ardhini muda mrefu.Dalili zake utaona matunda kama kuna sehemu zinakuwa nyeusi na panajaa majimaji ...dalili hii huenea sehemu kubwa ya tunda na baadaye tunda huoza.
Bacteria.
Madoamadoa ya bacteria kwenye matunda....huweza kutokea na kusambaa haraka wakati wa joto kali na unyevu kwenye udongo.Pia huu ugonjwa huweza kuenea kupitia mbegu.
No comments