KILIMO CHA PARACHICHI

 Tunda hili lina faida nyingi sana, mbali ya kutumika kama zao la kiuchumi lakini pia hutumika kuimarisha afya ya mwili

 

1. FAIDA ZA PARACHICHI UPANDE WA LISHE


– TUNDA LINA VITAMINI ZIFUATAZO

1. Lina Vitamini A-husaidia sana kuimarisha Macho kuona vizuri

2. Lina Vitamini B (B1-B12)- Husaidia sana mfumo wa misuli ya mwili kuwa sawasa na kuuepusha mwili na matatizo ya nerve

3. Lina Vitamini C-Husaidia sana upande wa kuimarisha ngozi, kwa sababu liko na mafuta, lina zaidi ya mara 4 ya virutubisho vya vitamini C vinavyopatikana katika machungwa

4. Lina vitamini D-ambapo husaidia sana kuimarisha mifupa ya mwili

5. Lina vitamini E-hii husaidia sana kuimarisha seli za uzazi, linasaidia sana kuongeza nguvu na utengenezwaji wa seli za uzazi

6. Lina vitamini K-Husaidia sana kuganda kwa damu, na kuongeza uzalishaji wa chembe hai nyekundu za damu

 

MADINI – (MINERAL ELEMENTS)

Ni tunda lenye :

1. Madini ya Chuma kwa wingi (Fe) – Haya husaidia sana utengenezwaji wa damu, na kuongeza uwezekano wa damu kuwa na oxygeni ya kutosha na kusafirishwa kwa urahisi

2. Madini ya Calcium – Lina madini ya calcium, yanayosaidia kama ufanyaji wa kazi wa seli hai za mwili

3. Lina virutubisho vingine vidogo vidogo vingi, vinavyotakiwa katika ufanyaji kazi mzuri wa selli hai za mwili

 

2. AGRONOMY YA PARACHICHI (HALI YA HEWA)


– Ni tunda linalopenda sana sehemu za baridi, maeneo kama ya Rungwe-Mbeya, Njombe, Makete, linastawi vizuri sana, na huwa na Fatty Contenty kubwa

JOTO : Nyuzi 15-25 Sentigrade

MUINUKO : Mita 1200-1800 kutoka usawa wa baridi

UDONGO : Uwe kichanga tifutifu (Sandy loam), usiotuamisha maji

 

AINA ZA PARACHICHI

1. Zipo aina za kiasili : Kila sehemu kuna aina za parachichi ambazo ni za asili ya eneo husika, parachichi hizi, huwa ndefu sana, na mavuno machache

2. Zipo aina za kisasa (Chotara) : Ziko aina nyingi sana za Parachichi chotara, na hizi hapa chini ni baadhi ya zile maarufu hapa tanzania

 

i. HASS

HASS AVOCADO
HASS AVOCADO

– Hii ni aina maarufu sana katika aina za parachichi

– Ni tunda linalokuwa na vipere vipere

– Limechongoka juu na chini

– Linahifadhika kwa urahisi

 

 

ii. Aina ya pili ni FUERTE

– Hili ni aina ya parachichi lenye ngozi laini saini, ngozi yake inateleza kama imepakwa mafuta

– Liko na mafuta mengi ila linawahi kuoza

– Ni zuri kwa matumizi ya kawaida , si kwa kusafirisha umbali mrefu

 

FUERTE AVOCADO
FUERTE AVOCADO

– Aina hii ikilimwa sehemu za miinuko na baridi sana, inafaa sana kutoa mafuta mengi yanayoweza kutumika kutengeza lotion na baadhi ya vyakula vya mifugo

 

iii. Aina ya tatu maarufu hapa tanzania inaitwa X- ikulu

– Ana hii ni maarufu sana kwa mikoa ya nyanda za juu kusini (Mikoa ya Njombe, Iringa, Mbeya na Ruvuma)

– Mti wa aina hii huwa na majani mapana kama mti wa embe

– Mti huu huchukua muda mrefu sana kustawi

– Tunda lake huwa ni kubwa, na lina gharama sana

 

UPANDAJI WA PARACHICHI

NAFASI KATI YA SHIMO NA SHIMO

– Umbali wa kutoka shimo hadi shimo ni MITA 7

– UMbali wa kutoka mstari hadi mstari ni MITA 7

Lakini kipimo hicho hapo juu kitategemea sana na aina ya udongo wa shamba lako , kwa udongo wenye Phosphorus kwa wingi (P), kipimo hicho hakifai, maana baada ya mika 3-5 miche ya mistari miwili inayofuatana itakuwa imekuatana katikati

 

– HIVYO NAFASI YAWEZA KUWA

8M X 8M – KWA NAFASI HII UTAKUWA NA MICHE 63 KWA EKA 1
AU 9M X 9M – KWA NAFASI HII UTAKUWA NA MICHE 49 KWA EKA 1
AU 10M X 10M- KWA NAFASI HII UTAKUWA NA MICHE 40 KWA EKA 1

UKUBWA WA SHIMO – Shimo laweza kuwa futi 2.5 x futi 2.5 x futi 2.5 = (sm 75 x sm 75 x sm 75) (Kimo x upana x urefu)

– Au kipimo cha futi 3 x futi 3 x futi 3= sm 90 x sm 90 x sm 90

 

MBOLEA

– Mbolea za kupandia zitakazohitajika , ni moja wapo kati ya hizi

– Samadi, Mboji, DAP, au TSP-Lakini ni muhimu kupandia mbolea asilia kama samadi ukachanganya kidogo na TSP au DAP

 

KIPIMO CHA MBOLEA

– Kama ni mbolea za asili (Samadi au Mboji)-Kiasi cha kilo 16 hadi 20 kinapaswa kiwekwe katika shimo miezi 3 kabla ya kupanda mche

– Kama utapandia mbolea za viwandani (TSP, DAP, Minjingu, NPK etc) kiasi cha gramu 100 hadi 200 kiwekwe kwa kila shimo, ichanganywe vizuri na udongo, kisha mmea uwekwe na kumwagiliwa

 

KUKOMAA NA KUTOA MAVUNO

– Parachichi hasa hizi za kisasa, hukomaa baada ya miezi 18 hadi 24

 

MAVUNO

– Kwa mara ya kwanza mti mmoja wa parachichi unaweza kukupa kati ya matunda 50 hadi 100 kwa mche mmoja.

– Mavuno hueongezeka kadri umri unavyoongezeka

– Mti wa parachichi ukifikia umri wa miaka 4 hadi 5, unakuwa full maturity, na hivyo mti mmoja unaweza kukupa hadi matunda 1200 kwa mwaka mzima ‘

 

FAIDA

Kwa kipimo cha mita 10 x mita 10, katika eka mmoja utakuwa na mita 40

– Kila mti baada ya mika 5 unaweza kukupa wastani wa matunda 1000

– Hivyo kwa miti 40, utakuwa na jumla ya matunda 40 x 1000= 40,000

– Kila tunda kwa bei ya shambani uuze tsh 250, na unamatunda 40,000

– Hivyo utapata jumla ya tsh 250 x matunda 40,000= 10,000,000 tsh (MILIONI 10)

 

 

MAGONJWA YA PARACHICHI


Parcahichi kama mimea mingine inashambuliwa sana hasa upande wa majani pamoja na matunda
. Yapo magonjwa ya majani, yanayosababishwa na fangasi/Ukungu, Algae, pamoja na wadudu, pamoja na lishe duni

JANI LA PARACHICHI LILILOSHAMBULIWA
JANI LA PARACHICHI LILILOSHAMBULIWA
JANI LILILOSHAMBULIWA NA ALGAE
JANI LILILOSHAMBULIWA NA ALGAE
UTITIRI MWEUPE KATIKA PARACHICHI
UTITIRI MWEUPE KATIKA PARACHICHI

 

AVOCADO LILILOSHAMBULIWA NA UTITIRI
AVOCADO LILILOSHAMBULIWA NA UTITIRI

 

 

2. MAGONJWA YA MATUNDA

Yasababishwayo na fangasi/Ukungu, Wadudu,na Lishe dunipia

UKUNGU / FANGASI
UKUNGU / FANGASI
TATIZO LA SCAB
TATIZO LA SCAB
THRIPS WA AVOCADO
THRIPS WA AVOCADO
Matunda yaliyoathiriwa na Thrips
Matunda yaliyoathiriwa na Thrips

 

 

DAWA

– Dawa za kutibu wadudu kama Karate, Matchi, Actellic 50 EC, za faa sana kumaliza wadudu katika mmea wa parachichi

– Dawa za Ukungu kama Ridomil Gold, Ebony 72 WP (Mancozeb na Metalaxyn), Ivory, na Nordox zaweza kutumika kumaliza matatizo ya ukungu

– Lishe ya mmea : Mbolea za kukuzia kama CAN, UREA NA SA (hasa kwenye maeneo yenye magadi kwa wingi, na chumvi nyingi) yaweza kutumika kubalane PH YA Udongo.

– Booster =Mbolea za majani, maua na matunda kama vile Polyfeed Starter, Polyfeed finisher, Wauxal macro mix, Potphos, au Multi K , Ni muhimu sana zikatumika wakati wa maua, na matunda ili kuzuia matunda ya parachichi kuabort (Fruit abortion) yakiwa machanga, pamoja na kuzuia matunda kudondoka yakiwa machanga.

HITIMISHO

Parachichi – Kama matunda mengine, ukililima kitaalamu, na ukaweka juhudi na maarifa linakutoa katika umaskini



No comments

Powered by Blogger.