KILIMO CHA ILIKI

 Iliki ni moja kati ya mazao ambayo yanatumika sana karibia kila siku kwenye matumizi ya nyumbani,utumika kama viungo kwenye chakula na pia utumika kama tiba ya magonjwa mbalimbali.na pia ni mmea mfupi ambao unatoa matunda kwa miaka mingi.


 AINA ZA ILIKI
Kuna aina mbili za iliki ambazo  ni
 malabar-huzaa kwa kutambaa ardhini na matunda yake ni madogo madogo.urefu wa mmea wa malabar ni karibia mita 3
  • mysore-matunda yake huzaliwa kwa wima,majani mapana na mmea una urefu zaidi ya mita3 

 MAZINGIRA NA HALI YA HEWA  
    • Huoteshwa kwenye maeneo yenye mvua 2500mm kwa mwaka
    • kivuli cha wastani
    • udongo wenye rutuba ya kutosha na ulio na unyevunyevu wa kutosha
  KUPANDA 
kunanjia mbili za kuotesha iliki unaweza kupanda mbegu au ukapanda miche midogo(spilits)
  • sia mbegu kwenye kitalu pandikiza mche shambani zikiwa na umri wa miezi 3-4 au zaidi zenye ukubwa wa sm 15 au zaidi  au tenganisha vimiche vinavyo zaliwa kwenye tunguu moja chini ya ardhi na pandikiza shambani.
  • tengeneza mashimo sm 60 x 60 na nafasi ya shimo panda miche kwenye mashimo. 

  KUTUNZA  
  • Weka matandazo
  • ondoa mashina ya zamani na yalio nyauka
  • rekebisha kivuli 
WADUDU NA MAGONJWA

Zuia wadudu waalibifu na magonjwa ili kupata mavuno mengi nayenye ubora
  • kuoza kwa majani-dhibiti kwa kupiga dawa zenye morututu k.m dithane m-45 
  • virus(mosaic virus)- dhibiti kwa kutumia aina inayo vumilia
  • inzi mafuta zuia kwa kutumia dawa za kuuwa wadudu insecticides 

 KUVUNA
  • Huchukua miaka 3 tangia kupandwa mpaka kuzaa na kuvuna pale unapopanda miche midogo
  • ukipanda mbegu huchukua miaka 4-5 mpaka kuvuna
  • matunda huvunwa hasa mwezi march na april
  • matundwa huvunwa na kukaushwa kwenye jua
na kipanda  kunauwezekana wa kuvuna 112-300 kwa heka na 45-120kg kwa eka ikiwa imekaushwa



No comments

Powered by Blogger.