JINSI YA KUTENGENEZA CHAKULA MBADALA KWA KUKU MINYOO (FUNZA)

 JINSI YA KUTENGENEZA MINYOO KWAAJILI YA KUKU



Kutengeneza minyoo ya chakula (red worms planning) Red worms planning ni utaratibu wa kuzalisha minyoo kwa ajili ya kuku na Samaki, Zipo hybrid Red Worms ambazo mara nyingi hununua sample kutoka nje ya nchi Kama Kenya,China au hapa Tanzania fuata hatua zifuatazo kuzalisha Red worms asilia.

1.Chukua mavi ya ngombe mapya au ngombe aliyechinjwa mavi ya tumboni

2.Kusanya Damu damu, ngozi, utumbo, magoroto, nyamanyama nk

3.Pakia kwenye kiloba au gunia kati ya chaguo A au B hapo juu

4.Chimba shimo la wastani kisha mwagia maji ndoo kubwa 4

5: Fukia hilo gunia na mwaga maji ndo 2 mara 1/2 kwa siku kwa muda wa siku 8/12

6: Baada Ya siku hizo kupita fukua na chepe utakuta minyoo mitupu ya kutosha kwa ajili ya chakula cha kuku au samaki na siku zinavyozidi kwenda ndo wanazidi kuzaliana na kuwa wakubwa

JINSI YA KUTENGENEZA FUNZA KWA CHAKULA CHA KUKU

Moja ya virutubisho muhimu kwa kuku ni protini ambayo unaweza ukawapa kupitia vyakula mbalimbali. Funza ni wadudu walio na protini nyingi ambayo inahitajika sana kwa ajili ya ukuaji wa kuku. Zipo njia mbalimbali ambazo zinatumika kutengeneza funza na hivyo kukupunguzia gharama za vyakula vya kuku. Jinsi ya Kutengeneza funza.
Tafuta kinyesi cha kuku au mavi ya ngo’mbe ambayo unaweza pata machinjioni au kuku wako mwenyewe. Chukua kinyesi weka kwenye kidumu kilichokatwa kisha weka pumba za mahindi kwa juu. Halafu weka maji kidogo ili kuvutia nzi waweze taga mayai hapo.
Utaendelea kuweka maji kwa siku mbili na kisha uache siku tatu. Siku ya nne au ya tano funza wataanza kutokea, wakusanye, waoshe na kisha wape kuku wale.

KANUNI AU HATUA ZAKUFUATA KUTENGENEZA MCHWA

1. Andaa mahitaji muhimu yanatakiwa -kinyesi kikavu cha ngombe au mbuzi -majani makavu,au mabua ya mahindi,maharage hata maranda unaweza tumia mojawapo au ukachanganya -chungu,au sufuria au box

2. Changanya vitu tajwa hapo juu vyote vizuri

3. Nyunyizia maji kila kilichomo kilowane kiasi

4. Weka mchanganyo wako kwenye chombo ulichokiandaa,chungu,sufuria au box

5. Chukua chombo hicho kakiweke sehemu ambayo unahisi mchwa wanaweza kupatika mfano,kichuguu, kwenye njia mchwa, sehemu nyingi ya ardhi kavu mchwa wanapatika

6. Acha chombo chako hapa kwa masaa 24, ila chombo umekiweka kwa kukifunika upande mmoja uwe umenyanyuka kidogo kuruhusu hewa kuingia kwenye mchanganyiko

7. Baada ya huo muda mchwa wengi watakuwa wamezalishwa ndani ya chombo chako

8. Chukua chombo kwa upesi kwa kukigeuza ili mchwa usirudi aridhini kisha kawape kuku wako, zoezi hili ni jipesi sana halihitaji wewe kutumia muda mwingi fanya kila siku ili vifaranga na kuku wako wastawi vizuri.

No comments

Powered by Blogger.