ULIMAJI WA MAKAKARA (PASSION)

Makakara ni matunda ya mviringo yapo ya rangi ya manjano na nyekundu kwa jina lingine huitwa Passion fruit hutumika sana katika utengenezaji wa sharubati  asili ya matunda  haya ni Bara la Ulaya

UILMAJI WA MAKAKARA

Makakara huanza kuandaliwa katika kitalu miche huoteshwa katika viriba vidogovidogo baadae huamishiwa shambani kira kiriba hupadwa mbegu mbili au tatu huanza  kuota katika kitalu ama viriba wiki mbili hadi tatu.

MBOLEA

Makakara  huhitaji udogo wenye rutuba ya kutosha maandalizi ya kitalu cha kuoteshea miche kinahitaji Kuandaliwa wiki moja kabla udongo uchanganywe na mbolea vizuri

UPANDAJI SHAMBANI

Makakara hupadwa kwa mstari mnyoofu ukumbwa wa shimo futi 1 kwenda chini na upana wa CM 60 umbali kati ya shimo na shimo ni mita 1 na nusu andaa miti mirefu kuweka katika kila shimo funga na kamba juu kati ya kila mti uliyouweka hii ni kwasababu makakara hutambaa.

UMWAGILIAJI

Makakara huhitaji maji ya kutosha ili yakuwa vizuri kama si msimu wa mvua na unatumia kilimo cha umwagiliaji mwagilia makakara asubuhi na jioni.

UPUNGUZIAJI WA MATAWI

Kama utahitaji matunda yako ya makakara kutoka makubwa unashauriwa basi kupunguza matawi machache ili kuluhusu matunda ya makakara kuwa makubwa.

MAVUNO

Baada ya miezi sita hadi saba  matunda huwa tayali sasa shambani kama ilitumia mbegu za muda mfupi lakini mbegu nyingine ambazo hazijaboleshwa huchukua miezi kumi hadi kumi na miwili ndo kuanza kutoa matunda.

CHANGAMOTO ZA MAGONJWA

Uonapo dalili zisizo nzuri basi ni vyema kufika kwa wataalamu mabwana shamba .

No comments

Powered by Blogger.