NJINSI YA KUWALISHA KUKU WA MAYAI

Kuku wa mayai hulishwa kwa utaratibu maalumu katika ukuwaji wao kuanzia akiwa kifaranga adi akifikia muda wakuanza kutaga kuku wa mayai huanza kutaga akiwa na miezi mitano kama akizingatiwa vizuri katika ulishaji.

a) Kuanzia wiki ya kwanza  hupewa chakula aina SUPER STARSTER gramu  11

b) Wiki ya pili gramu 22

c) Wiki tatu virafanga hupewa chakula cha aina ya CHICK STARSTER gramu 27

d) Wiki ya nne gramu 32

e)  Wiki ya tano gramu 38

f)  Wiki ya sita gramu 40

g)  Wiki ya saba gramu 45

h)  Wiki ya nane gramu 50

I) kuanzia wiki ya tisa hubadilishwa tena chakula huanza pewa chakula aina ya GROWER MASH gramu 56

j) Wiki ya kumi gramu 62

k) Wiki ya kumi na moja gramu  65

L) Wiki ya kumi na mbili gramu 60

m) Wiki ya kumi na tatu gramu 64

n)  Wiki ya kumi na nne gramu  68

O)  Wiki ya kumi na tano gramu  72

p) Wiki ya kumi na sita gramu  76

q) Wiki ya kumi na saba gramu  82

r) Wiki ya kumi na nane gramu 86

Kuanzia wiki ya kumi na tisa hadi wiki ya arobaini hapa kuku huanza kutaga kwa wingi hupewa chakula aina ya LAYERS PHASES 1


Kuanzia wiki hiyo ya kumi na tisa kila kuku atakula gramu 96 utamuongezia kila wiki gramu kumi na mbili mpaka wiki ya 27

Kuanzia wiki  ya ishirini na nane hadi arobaini kuku hupunguza kasi ya utagaji ovyo hupewa chakula aina ya LAYERS PHASES 2 wanapofikia muda wa wiki arobaini unashauriwa uwauze watakuwa wamepoteza asilimia kubwa ya utagaji mayai

No comments

Powered by Blogger.