BANDA BORA LA KUKU


acebook

• Banda bora lazima liwakinge vyema kuku dhidi ya upepo, hivyo banda lazima lizungushiwe kuta fupi ili kuwepusha na pepo za mara kwa mara.

• Ili kuwakinga kuku dhidi ya mvua inapasa kujenga mapaa mazuri na marefu, mapaa yanaweza kujengwa kwa majani au mabati.

BANDA BORA LA KUKU
BANDA BORA LA KUKU

• Kuwaepusha kuku dhidi ya jua kali banda lijengwe kwa mapaa marefu, mapaa yanayojengwa kwa kutumia majani na vipande vya mianzi kwa sababu ni rahisi na yanaruhusu mzunguko wa hewa safi lakini hayadumu kama ilivyo mapaa ya bati ambayo pia ni ghali mno. Kupanda miti karibu kutapunguza joto ndani ya mabanda. Kuku pia wanahitaji banda lenye nafasi ya kutosha kuweza kutembeatembea na inayowaruhusu kula chakula, kunywa maji, kutaga na kuangua mayai kirahisi

BANDA BORA
BANDA BORA
BANDA LIWE KARIBU NA MITI
BANDA LIWE KARIBU NA MITI

 Vilevile kuku wanahitaji banda lenye kuruhusu hewa na mwanga wa kutosha. Hii ni kwa sababu wakati wa majira ya joto na nyakati za mchana mapaa ya bati hufanya mabanda kuwa na joto kali. Vilevile kuruhusu vichaka karibu na banda kutazuia mwanga na mzunguko mzuri wa hewa safi ya kutosha. Itabidi ifahamike kwamba kuku hawatoi jasho na hivyo huondosha joto la ziada la miili yao kwa kuacha midomo wazi na hii ni dalili ya kuwa hawajihisi vyema na hali hii huwazuia kula chakula cha kutosha hivyo kusababisha washindwe kukua na kutoa mayai mengi.

LIRUHUSU KIVULI
LIRUHUSU KIVULI

 Jua lisiruhusiwe kupenya ndani ya banda wakati wa mchana. Mwelekeo wa kuta ndefu za banda ziwe Mashariki-Magharibi. Mwelekeo wa namna hii utaruhusu kivuli muda mrefu wa jua kali la mchana. Pia ili wawe katika hali nzuri kuku wanahitaji sehemu ya giza na iliyojuu kulala au waweza kujenga sakafu iliyoinuka wa sentimita 60 toka ardhini.

 Kuku hawapendi unyevunyevu, sakafu chafu na inayotoa harufu mbaya. Hata Vifaranga hawawezi kuhimili unyevunyevu na baridi kwa vile hali hiyo huweza kusababisha wakapata magonjwa.

MFANO WA MABANDA MAZURI YA KIENYEJI
MFANO WA MABANDA MAZURI YA KIENYEJI

 Kuta za banda zijengwe kwa kutumia vipande vya mianzi, mabati yaliyokwishatumika, au miti na udongo.

 Kutengeneza msingi wa banda kwa mawe ili kudhibiti uharibifu unaosababishwa na vicheche, nguchiro, mbwa wanaozulula ovyo na panya. Lakini sehemu ya ndani ya banda lazima iwe nyororo.

 Weka majivu ndani ya banda au tumia dawa ya Akheri Powder kuwakinga kuku dhidi ya mashambulizi ya siafu, viroboto, chawa na utitiri.

 Banda angalau liwe na kuta fupi zenye kina cha mita 1.8

UZIO MUHIMU KATIKA BANDA LA KUKU
UZIO MUHIMU KATIKA BANDA LA KUKU

KUPUNGUZA MLIPUKO WA MAGONJWA

 Sakafu ifunikwe kwa maranda ya upana wa sentimita 5 na yasambazwe vizuri. Maranda lazima yabadilishwe mara kwa mara yanapochafuka, yanapopata unyevu au ukungu kuepusha magonjwa.

 Pia banda laweza kujengewa vichanja ili kuruhusu vinyesi kudondoka ardhini. Na sehemu ambayo vinyesi hudondokea chini ya banda isiweze kufi kiwa na kuku kwa sababu mara nyingi vinyesi hubeba vijidudu vinavyosababisha magonjwa.

 Mabanda ya miti yanahitaji uangalifu wa kina kudhibiti vimelea kama utitiri, kupe na chawa. Hivyo miti ipakwe mafuta machafu, pia mabanda na vyombo vinavyotumika visafi shwe na kupuliziwa dawa (disinfenctant) kama V-RID kila mara pia waweza kutumia chokaa hasa kabla ya kupokea mkupuo mpya wa kuku.

 

KUWAPATIA KUKU HEWA SAFI

Banda lapasa kuwa na kuta mbili imara zenye urefu wa mita 1 na madirisha ya waya au vipande vidogovidogo vya mianzi kwa juu. Elekeza kuta hizi mbili mbali kutoka mwelekeo wa upepo.

 

KUWAPATIA KUKU MWANGA

Ujenzi wa paa la banda lenye kina cha mita 1.8 kutoka chini una faida zifuatazo: kutoa kivuli, mkulima anaweza kuingia kirahisi ndani ya banda, pia kama ikiwezekana liwe na kuta zenye uwazi upande unaopochomoza jua. Likinge banda (Tengeneza kivuli) upande ambao jua linazamia.

 

NAFASI KWENYE SAKAFU KWA KUKU

Wacha nafasi ya kutosha kwa ajili ya malishio, m a n y w e s h e o , matagio na kwa kuku kuweza kutembea tembea . Nafasi inayopendekezwa kwa kuku 4 hadi 6 ianzie mita mraba moja.

No comments

Powered by Blogger.