KILIMO CHA MAHARAGE
Kuna aina nyingi za maharage ambazo zinaweza kupandwa kwa mfano (Rojo, Mshindi, Pesa, SUA 90 na Canadian wonder) ambazo ni mbegu zilizoboreshwa.
KIASI CHA MBEGU KWA EKARI
Kilo 15 hadi 20 za mbegu za maharage zinatosha kuotesha shamba la ekari moja shamba,
UPANDAJI WA MBEGU
Namna ya upandaji wa mbegu za maharage
Inashauriwa kupanda maharage katika umbali wa sentimita 50 (mstari kwa mstari) na sentimita 20 (mmea kwa mmea), panda mbegu mbili za maharage katika shimo moja, mbegu zinaweza kupandwa katika umbali wa sentimita 3 Chini ya Udongo.
MBOLEA
Mimea ya maharage inahitaji virutubisho vya kutosha kutoka kwenye udongo ili kuweza kukua na kuzalisha matunda yenye afya.
Ni vizuri kutumia mbolea hai ambazo zinasaidia viumbe hai huweza kukua na kuendeleza kurutubisha udongo, kwa mfano mizizi ya maharage husaidiana na viumbe hai (nitrogen fixing bacteria) waishio kwenye udongo kutengeneza nitrogen.
Nashauri Mkulima kutumia mbolea ya DAP Kuoteshea maharage: DAP yaweza tumika kipindi cha kusia mbegu au wiki 1 mara baada mche kuota.
UDHIBITI WA MAGUGU
Shamba lililokuwa safi dhidi ya magugu |
Inashauriwa kupalilia shamba mara tu magugu yanapotokea na kabla mimea haijatoa maua.
Palilia kwa jembe la mkono au kung'olea magugu na maotelea yote shambani, waweza tumia kemikali kudhibiti uotaji wa magugu kabla ya kupanda maharage shambani.
KUKABILIANA NA VISUMBUFU SHAMBANI
Maharage hushambuliwa na wadudu na magonjwa mbalimbali.
Miongoni mwa njia
za kuzuia, kukinga na kufukuza wadudu ni kuhakikisha kuwa mimea
ipo katika hali nzuri (imepaliliwa, nafasi ya kutosha na haijaharibika).
Pia kubadilisha aina ya mimea inayopandwa kwenye shamba moja mara
kwa mara husaidia kupunguza uwezekano wa wadudu kuongezeka.
KILIMO ANUAI (Organic Farming)
Kwa baadhi ya wadudu kama vile viwavi (African Ballworm) na magonjwa ya Fangasi huweza
kudhibitiwa kwa kutumia muarobaini au vitunguu saumu.
Maji ya muarobaini ni dawa nzuri sana kwaajili ya kufukuzia wadudu na kudhibiti magonjwa ya Fangasi na haina madhara yoyote kwa binadamu.
KEMIKALI: Tumia Viuatilifu kudhibiti magonjwa na wadudu wanaotokea shambani
VIUWA DUDU MADHUBUTI:
Duduba, dusuall, Duduwill, Wilcron, Cutter, Wiltigo, Liberate N.k
VIUWA KUVU (MAGONJWA YA FANGASI): Innovex, buctril, ridomil, wilthane,Superwil, Folicur n.k
MAHARAGE KUKOMAA NA KUVUNWA.
Maharage ya kijani/ Mabichi yanatakiwa yavunwe kabla punje za maharage hazijakuwa sana. Hii ni kati ya wiki 7-8 baada ya kupanda. Maharage makavu huvunwa mara tu kiasi cha kuridhisha cha kukomaa na kukauka kinapokuwa kimefikiwa.
Asilimia 80 ya maharage yakishakomaa na kuanza kubadilika rangi (kukauka) au kwa aina nyingine kusinyaa yanakuwa tayari kwa mavuno.
Kwa kawaida mmea wote hung’olewa na kuwekwa juani ili uendelee kukauka kisha maharage hutolewa kutoka kwenye mmea na kuendelea kukaushwa ili kupunguza matatizo wakati wa kuhifadhi.
Baada ya kukauka hadi kufikia angalaua asilimia 12 ya unyevu, maharage yanatakiwa yahifadhiwe kwenye chombo chenye mfuniko kama vile ndoo ya plastiki au pipa na kuendelea kuyaangalia mara kwa mara ili kuhakikisha kuwa wadudu hawajaingia na kisha kuyafunika tena.
VIUWA KUVU (MAGONJWA YA FANGASI): Innovex, buctril, ridomil, wilthane,Superwil, Folicur n.k
MAHARAGE KUKOMAA NA KUVUNWA.
Maharage yaliyokomaa na kukauka vizuri |

No comments